Mututho aunga mkono kutimuliwa kwa NTSA barabarani

Aliyekuwa mwenyekiti wa NACADA Bw John Mututho ameunga mkono pendekezo la Rais Uhuru Kenyatta la wiki kadha zilizopita la kufurusha maafisa wa mamlaka ya uchukuzi na usalama wa kitaifa (NTSA) barabarani. Rais Kenyatta aliagiza maafisa wote wa NTSA kuondoka barabarani, majukumu yao yakipokezwa maafisa wa polisi wa trafiki. “Waondoke waachie maafisa wetu wa trafiki wafanye kazi yao barabarani,” amesema Bw Mututho mapema Jumamosi akiongea mjini Nakuru. Mamlaka ya NTSA imekuwa ikituhumiwa kuzembea kazini na kushindwa kudhibiti viwango vingi vya ajali ambavyo vimekuwa vikitendeka nchini, na kusababisha vifo vya ajali barabarani. Bw Francis Meja ndiye mwenyekiti wa NTSA.

Kwa upande wake Mututho ni kwamba barabara zinahitaji wafanyakazi waadilifu na wanaoelewa majukumu yao. “Tunataka watu wanaofanya kazi ipasavyo, barabara hizo huhusisha maisha ya binadamu. Kwa nini yachezewe?” akataka kujua. Kipindi cha mwezi Desemba 2017 pekee, zaidi ya abiria 200 walifariki kwenye ajali mbaya barabarani. Salgaa, Sachangw’an na Mai-Mahiu katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru-Eldoret ni maeneo ambayo yameorodheshwa kuwa hatari nchini kwa watumizi wa barabara. Mwaka 2017, NTSA ilipiga marufuku safari za masafa marefu usiku ambapo matatu hizo hulazimika kutia nanga safari saa kumi na mbili za jioni. Hata hivyo, mapema wiki hii mwenyekiti wa NTSA Bw Francis Meja alisema marufuku ya usiku ilikuwa ya muda tu. Aliongeza kuwa, wanatarajia kuanza safari hizo baada ya muda wa wiki mbili zijazo. Bw Meja alisema waziri wa Uchukuzi na Usalama watatoa mwelekeo wa safari za usiku. Pia Alhamisi juma hili, mwanaharakati Okiya Omtatah aliwaongoza wasafiri na baadhi ya kampuni za usafiri wa umma kumshawishi Jaji Enoch Chacha Mwita wa mahakama kuu kuondoa kwa muda marufuku ya safari za usiku. Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi inaongozwa na waziri James Macharia, huku ile ya Usalama ikiwa chini ya Dkt Fred Matiang

Visit JOMEC Website