Mapendekezo ya kupimwa wanafunzi kubaini iwapo wanatumia mihadarati

Hatua ya mwenyekiti wa NACADA John Mututho ya kupendekeza kupimwa kwa wanafunzi kubaini iwapo wanatumia dawa za kulevya imepokelewa vyema na baadhi ya wazazi kaunti ya Mombasa. Wakizungumza na mwanahabari wetu wamesisitiza kukamatwa kwa walanguzi wa kuu wa dawa za kulevya kwani ndio wanaochangia kuongezeka kwa utumizi huo jambo linalochangia matokeo duni hapa mkoani. Wachira Benson mmoja wa wakaazi hao amesisitiza kuwa utumizi wa dawa hizo unaharibu akili na afya ya wanafunzi na hatimaye kukosa kufanya vyema katika mitihani na maisha kwa jumla.

Aidha amejitoa mfano na kusema kuwa alianza kutumia bangi akiwa darasa la saba jambo lililomfanya kutofanya vyema katika masomo yake. Mwenyekiti wa NACADA John Mututho alisisitiza kushirikiana na wizara ya afya pamoja na elimu kukabiliana na tatizo hilo na shule zitakazo patikana na watumizi wa dawa hizo zitafungwa.

Visit JOMEC Website