Mututho ataka muundo wa barabara ya Salgaa kurekebishwa kupunguza ajali

Aliyekuwa Mwenyekiti wa NACADA John Mututho amesema muundo wa barabara ya Salgaa unafaa kurekebishwa ili kupunguza visa vya ajali katika eneo hilo. Hii ni baada ya watu wanane kufariki kwenye barabara hiyo katika visa viwili vya ajali mwishoni mwa wiki.

Kwa habari husika, watu 32 wamefariki kutokana na ajali za barabarani mwaka huu. Francis Mejja kutoka mamlaka ya usalama barabarani amesema idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka kutoka 80 hadi zaidi ya watu 200 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Visit JOMEC Website